Ususi ni miongoni mwa ajira iliyoajiri maelfu ya akinamama nchini huku wengi wakiendesha familia zao na kusomesha watoto wao kwa kazi hiyo. Lakini fani hiyo haijawahi kurasimishwa ipasavyo licha ya kuwa kimbilio la wanawake wengi wanaopenda kupendeza.
Kwa kulitambua hilo, Jokate Mwegelo kupitia brand yake ya Kidoti, akishirikiana na kipindui cha Leo Tena cha Clouds FM, wamekuja na kampeni iitwayo Msusi Wao yenye lengo ya kuwawezesha kiuchumi wasusi nchini.
Jokate akiwa na wadhamini na washiriki wa kampeni hiyo wakati wa kuitambulisha Jumanne hii
“Kiukweli wasusi walioweza kufika licha ya muda mdogo mmenipa moyo. Sasa basi siku zenu za kuchuliwa poa kama wasusi ziishe leo. Ujuzi wako huu ndio ajira yako ndio kitu kitakocholisha familia yako na kuiendeleza taifa letu. Tuipe thamani, tuwe wabunifu zaidi na kutengeneza fursa zaidi,” ameandika Jokate kwenye Instagram.
Chini ni picha zaidi za Jokate wakati wa kutambulishwa kwa kampeni hiyo.
Katika kampeni hiyo, Jokate ameazimia kuwasaidia wasusi ambao hawana saluni maalum za kufanyia kazi zao.
“Kila moja wetu ana wajibu wa kumuinua mwenzake kutokana na uwezo wake na kile kidogo alichojaaliwa,” anasema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni