Mkali wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz Alhamisi hii siku moja kabla ya birthday ya mama watoto wake Zari, ameonyesha nyumba ya familia aliyonunua Afrika Kusini.
Muimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii wachache wenye mafanikio makubwa hapa nchini, hakuweka wazi nyumba hiyo imegharimu kiasi gani kuinunua.
“Wanakazana kujisifu matajiri Ilhali watoto zao wanaishi kwenye Nyumba zakupanga. Halafu leo yule yule wanaemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa masikini, kajawa na shida, Kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora kama wanayoyatamani. Heri ya siku ya Kuzaliwa Mama tee wangu. Nakupenda sana na unalifahamu hilo, natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South Africa. Nasubiria kwa hamu kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho (leo) Zanzibar,” Diamond aliandika instagram.
Muimbaji huo amevunja zile tetesi za kwamba huwenda hayupo sawa na mama Tiffah baada ya mrembo huyo siku chache zilizopita kudai amekuta hereni za mwanamke mwingine chumbani kwake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni