Msanii Mataluma aliyewahi kufanya vizuri na ngoma zake kama ‘Mama Mubaya’ ‘Kariakoo’ wakati huo akiwa THT lakini ghafla amepotea, amepanga kurejea kwa kishindo.
Akiongea na glovetz Mataluma amesema muda wote huo alikuwa akifanya biashara yake ya mkaa iliyomweka busy, lakini sasa imedoda.
“Unajua siyo kama nilikuwa sifanyi muziki, hapana nikuwa nafanya na nilikuwa narekodi na ngoma zipo zingine nimefanya na msanii Man Fongo ambaye sasa hivi anafanya vizuri. Na pia nilifanya na Msaga Sumu, hawa wote nimefanya nao kazi hata kabla hawajaaanza kufanya vizuri na huu mUziki wa Singeli,” amesema.
“Sasa narudi rasmi kwenye muziki baada ya biashara zangu kukwama kutokana na serikali hii ya awamu tano, imeweka utaratibu wa kuwa na vibali maalumu ili kufanya biashara ya mkaa,” ameongeza.
“Narudi na ngoma nimefanya kwa Pancho ambayo ina baadhi ya mchiriku, najipanga kuweka mambo sawa. Nipo mwenyewe kwa sasa sina menejimenti, ila ikitokea mbona itakuwa poa maana muziki sasa hivi umebadilika na umekuwa biashara,” amesisitiza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni