burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

10 Sep 2016

Y-Tony aelezea kufananishwa kwake sauti na Rich Mavoko

Kwa muda mrefu kumekuwepo na mfanano unaotajwa kuwepo kati ya muimbaji wa ‘Wivu Wangu’ Y-Tony pamoja na muimbaji wa ‘Ibaki Story’ Rich Mavoko.
2
Ili kupata ukweli wa kinachosema, nilizungumza na Y-Tony kutaka kujua anasemaje. Alikiri kuwa yeye na Mavoko wana historia ya kuwa washkaji na kuhustle pamoja.
Muimbaji huyo amedai kuwa yeye na Mavoko ni marafiki wakubwa lakini ni kazi tu ndivyo ambavyo vimewatengenisha. Amedai kuwa suala la kufanana na Rich ni kitu ambacho kwa upande wake hakioni.
“Mimi sina sauti nyembamba, nyimbo zangu zote ukisikiliza na Rich ni tofauti,” amesema Y-Tony. “Lakini kuna vitu fulani mashabiki wanapendaga kwamba wao wenyewe wanavyosema huwezi kuwakatalia. Wape mashabiki nafasi ya kuamua wanachokisema lakini mwisho wa siku kazi nzuri kinajieleza.”
Mtazame zaidi hapo juu akielezea zaidi kuhusu suala hilo na mambo mengine

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni