Hebu fikiria Dunia Njia na Usilie vikiunganishwa na kuwa wimbo mmoja itakuaje?
Au Bushoke na Christian Bella wakiingia studio kufanya wimbo wa pamoja! Hicho ni kitu ambacho mashabiki wengi wanakitamani.
Akiongea na mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, Dj Rodger, Bushoke amesema amekuwa akiambiwa na watu wengi afanye wimbo na Bella na kwamba mpango huo upo.
Bushoke amedai kuwa mashabiki wanaamini kuwa collabo yake na Bella itakuwa tofauti na itafanya vizuri pia kajipanga na hii game ya sasa na kawaaomba mashabiki wake kuwa tayar kuipokea collabo hio matata soon itakuja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni