Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol amesema anatarajia kuja na remix ya wimbo wake, Moyo Mashine akiwa na msanii wa Nigeria, Chidinma.
Hadi sasa ‘Moyo Mashine’ umekuwa wimbo wa Ben Pol wenye mafanikio makubwa.
Chidinma
Muimbaji huyo, ameiambia glovetz kuwa remix hiyo itakuwepo kwenye album yake mpya.
“Ngoma ambayo inakuja ni Moyo Mashine remix ambayo nimefanya na Chidnma kutoka Nigeria,” amesema. “Nilimsikilizisha nyimbo nyingi lakini aliupenda huo, nikaona sawa,” ameongeza.
“Na pia kuna nyimbo nyingine tena nimefanya naye muda wake ukifika nitauzungumzia huo wimbo. Na hizi nyimbo zote zitakuwa katika album yangu mpya ambayo nategemea itatoka baada ya mwezi Disemba.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni