burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

17 Sep 2016

Kuna kipindi nafikiria ingekuwa inaruhusiwa binti Nyange ningejioa mwenyewe – Dayna Nyange

Msanii anayefanya vizuri na wimbo ‘Angejua’ amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa amejifunza kutoweka wazi maswala ya mahusiano yake ya mapenzi.
Dayna
Muimbaji huyo amesema anashindwa kumweka wazi mpenzi wake kwa kuwa huyo aliyenaye hana uhakika kama ndo atakuwa wake wa milele kwa kuwa tayari ameshapitia wengine wa namna hiyo.
“Kuna wakati hata mimi natamani kuwa na mpenzi wangu nikamweka hivi licha hata ya kumweka insta lakini nitoke naye niwe free, lakini kuna mazingira ambao nayaona sijui ni malezi unajikuta una hofu, sawa huyu ni mpenzi wangu, ukiangalia huyu sio mtu wa kwanza nimekutana naye, nimeshakutana na mwingine lakini kwa mipango ya ibirisi au Mungu sijui tukaachana, kama unaweza kuachana naye basi haimaanishi kwamba huyo uliyenaye ndo utakuwa naye maishani. Kikubwa unaingia kwenye mahusiano ni kumshukuru Mungu na kuomba heri, kwa sababu hakuna haijue kesho,” alisema Dayna alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza, “Na kutokumpost mpenzi wangu instagram watu wakamjua ni sihitaji kutengeneza picha fulani kwamba, Dayna yupo na fulani, Dayna wataanza kumchunguza kwa hiki, yaani kuna vitu vyangu vipo private sipendagi kuviweka wazi, na ukiangalia pia vitu ukiviachia vikizidi sana, unaweza kujikuta unakuwa na stress sana, najua kuna wakati maisha ya mapenzi yanakuwa na stress sana, yaani kuna wakati mpaka unajiona ingekuwaga inaruhusiwa binti Nyange ningejioa mwenyewe,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni