Msanii wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Siwezi’ Barakah Da Prince amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi mpya.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya, amesema amesikia kilio cha mashabiki wake.
“Nachopenda kuwaambia mashabiki wangu ndani ya hizi siku mbili mtafurahi sana, mmelalamika sana,” alisema Barakah Prince kupitia video aliyoweka katika mtandao.
Muimbaji huyo tayari amefanya kolabo na mkali wa wimbo Aje, AliKiba na tayari ‘wameshaiperform’ mara moja katika show ya Fista Mwanza.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo, amewaomba radhi wale aliowakosea huku akiomba baraka kutoka kwa mashabiki wake katika safari yake ya kuupeleka muziki katika level nyingine.
“It’s almost a year tangu nilipoachia kazi yangu ya mwisho ‘Siwezi’. Katika kipindi hiki nimepitia mambo mengi sana, nimekuwa kiakili, kifikra na kisanaa na sasa nipo tayari kuianza safari mpya. Kufika hapa leo haikuwa kazi rahisi, pamoja na kipaji changu nilichojaaliwa na Muumba, lakini labda bila usaidizi mkubwa niliopata kutoka kwa baadhi ya watu, pengine nisingekuwa hapa leo, hivyo ningependa kuwashukuru wazazi wangu na familia yangu, #TetemeshaRecords #RoyalNsyepa ,Media zote, Radio & TV Personalities, Waandishi wa habari na msingi mkuu wa sanaa yangu na mashabiki wa muziki wangu. Asanteni sana kwa support yenu na kama kuna yoyote niliwahi kumkosea naomba #Nisameh, kukosea kwangu ndio ukamilifu wangu kama mwanaadamu,” aliandika Barakah instagram.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni