Rapper Stamina baada ya kufanya vizuri na albamu yake ya ‘Mt Uluguru’ anajipanga kuachia albamu mpya mwezi Disemba ambayo itakuwa na nyimbo 15
Akiongea na glovetz wiki hii, Stamina amesema tayari ameshamaliza kurekodi nyimbo zote za albamu hiyo na sasa ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kutoka.
“Albamu mpya kwa sasa ipo jikoni kwa Rash Don, nimeshamaliza kurekodi na Disemba inaingia sokoni,” alisema Stamina. Nashukuru mungu hii ni tofauti ili iliyopita, mapaka sasa ninapozungumza na wewe tayari kuna wadhamini wamejitokeza kwa ajili ya usambazaji pamoja na kuandaa matamasha ya uzinduzi,”
Rapper huyo amesema nyimbo hizo 15 amefanya na maproducer tofauti tofauti ili kupata ladha tofauti katika kila wimbo.
Albamu iliyopita ya ‘Mt Uluguru’ iliuza nakala 9,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni