Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.
Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliongea na Amplifaya ya CloudsFM na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Kigamboni Dar es Salaam.
Sasa headlnes za msanii huyo zimerudi tena baada ya Mkurugenzi wa kituo cha Sober House Nuru kufunguka kusema kwamba ameondoka bila kumaliza matibabu yake.
‘Unajua wakati mwingine tunapata matatizo kuwachukua watu maarufu ndio kama hivyo mtu anaamua kuondoka hata hajamaliza matibabu sisi tumefanya kazi kwa miaka mingi na tunajua jinsi ya mtu aliyeathirika na madawa ya kulevya anatakiwa apewe nini’
- ‘Sijui mimi tu ndio nalalamika Sober House bali watu wengi maarufu ndio wanatupa shida sana, sasa Ray C ameondoka hapa amekaa miaka mitatu na alitakiwa akae hata mwaka ili aweze kupata matibabu vizuri lakini imekuwa tofauti mara napigiwa simu naambiwa Ray C ameondoka kwenye Sober House yangu’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni