Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amefunguka kwa kuitaja kazi aliyotamani kuifanya kama asingekuwa mwanamuziki.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Dj Show cha Radio One, Nico Track, rapper huyo amedai kuwa angekuwa ni mkufunzi wa chuo kikuu.
“Hamna kazi ninge-enjoy kuifanya kama ningekuwa Professa wa chuo kikuu, sijawahi kutaka kuwa daktari, rubani, mwanasheria wala yeyote,” amesema Fid Q.
“Mimi nimekuwa mtu wa kupenda vitu vya academy na vitu vingine vya masuala ya uelimishaji ndio maana hata kwenye muziki sifanyi Entertainment mimi nafanya Edutainment. Kwahiyo mimi ni Edutainer si Entertainer,” ameongeza.
Fid Q ni mmoja kati ya wasanii wenye uwezo wa kuchana na kuandika mistari yenye misamiati ambayo ndani yake imebeba ujumbe mzito.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni