burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

10 Sep 2016

Jimmy Chansa: Natamani kumshirikisha Vanessa Mdee ‘amekamilika kila idara’

Muimbaji wa ‘We Mchoyo’, Jimmy Chansa amedai kuwa Vanessa Mdee ndiye msanii anayependa kuja kumshirikisha siku za usoni.
jimmy-2
Jimmy ameiambia Bongo5 kuwa Vanessa ni msanii aliyekamilika katika idara zote.
“Napenda style yake ya uimbaji. Halafu mimi kwa upande wangu [Vanessa] ni complete set ya msanii,” anasema Jimmy/. “Kwasababu msaniii kuimba ni sehemu ndogo sana, kuwa na sauti nzuri ni asilimia kama tatu katika mia, kuna muonekano, kuna jinsi unavyojiweka mwenyewe, personality, unavyoongea na watu, unavyojibu maswali, mimi namkubali zaidi Vanessa Mdee.”
Jimmy amesema anaamini kuwa Vanessa atakuwa anamfahamu kwakuwa wimbo wake wa kwanza ‘Sorry’ Jux anaipenda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni