Producer Mesen Selekta wa De Fatality studios amesema kuwa yeye ndiye producer pekee anayetengeneza muziki halisi wa Singeli.
Akiongea katika kipindi cha The Base cha ITV, Mesen amefunguka kuwa maproducer wengi wanajaribu kutengeneza Singeli lakini wanakosea kwa kufananisha muziki huo na mnanda.
“Unajua kuna muziki unaitwa Singeli, kuna mnanda na ladha, sometimes kuna baadhi ya producer wanajaribu kutengeneza Singeli lakini inakuwa sio Singeli, unakuwa unasound kama mnanda au ladha na ndio maana mpaka sasa hivi Mesen anabaki kuwa producer pekee wa Singeli,” alisema.
Mesen ametayarisha hits nyingi za Singeli zikiwemo ‘Hainaga Ushemeji ya Man Fongo, ‘Sembe Tembele’ ya Sholo Mwamba na wimbo mpya wa Profesa Jay, Kazi aliomshirikisha Sholo Mwamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni