Msanii wa muziki kutoka visiwani Zanzibar, Baby J amesema ushirikiano kati ya wasanii wa kike ndio kitu pekee ambacho kitawakomboa wasanii wengi wa kike na kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimataifa.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya kazi chini ya Mkubwa Fella, ameiambia glovetz kuwa wasanii wengi ambao wanafanya vizuri wanawavimbia wenzao hali ambayo amedai inapoteza ushirikiano.
“To be honest wasanii wa kike hatuna ushirikiano, wasanii wakike hatupendani hasa hawa ambao wanafanya vizuri au umeshapata nafasi,” alisema Baby J. “Wenzetu wakiume wanashirikiana hata japo kwa uongo lakini tunaona wanashirikiana, lakini wasanii wa kike ushirikiano ni mdogo sana na kinachosababisha kuna ile chembe chembe ya ‘ujana jike’, yaani kuna yale mambo fulani wa kike ambao tunao,”
Muimbaji huyo amesema ushirikiano kati ya wasanii wa kike kunaweza kusaidia kuongeza idadi ya wasanii wa kike wataofanya vizuri kwenye muziki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni