Wataalam wanasema kulala bila nguo kuna faida nyingi, tena nyingi za kukupa utajiri. Sio utani eti! Lakini wanaolala kwa mtindo huu ni asilimia 8 tu.
1. Unapata usingizi mtamu ukilala bila nguo
Kwa mujibu wa utafiti wa chuo kikuu cha Rochester, unapolala, ubongo wako hutoa protini zenye madhara kutoka kwenye mishipa yake ambazo huzaliwa kwa shughuli za kawaida unapokuwa umeamka.
Mchongo hapa ni kwamba, ubongo wako utaweza kutoa protini hizi vyema unapopata usingizi wa kutosha. Unapokosa usingizi mzuri, protini hizi hubaki kwenye seli za ubongo wako na kukupotezea uwezo wako wa kufikiri.
Utafiti mwingine wa chuo kikuu cha Amsterdam unadai kuwa kupunguza joto la ngozi yako huongeza ubora wa usingizi na kupunguza idadi ya kuamka usiku. Kuvua nguo, ni njia nzuri ya kupunguza joto la kwenye ngozi bila kubadilisha joto la chumba chako.
2. Kulala bila nguo kunapunguza stress
Inajulikana kuwa stress za muda mrefu si nzuri. Huathiri kinga zako mwilini na kuongeza hatari za kupata ugonjwa wa moyo, depression, na kunenepa. Kupumzika ipasavyo husaidia kiwango chako cha stress bila kuzingatia kinachotokea kukuzunguka. Kama ilivyoeleza hapo juu, kulala bila nguo kunakupa njozi tamu usiku.
3. Kulala bila nguo ni afya
Kulala bila nguo kuna orodha ndefu ya faida ikiwemo kupunguza uzito. Kulala bila nguo kunaongeza mzunguko wa damu mwilini kitu ambacho ni kizuri kwa moyo na misuli yako.
4. Kulala bila nguo kunakuongezea hali ya kujiamini
Kujiamini si tu kujisikia vizuri, ni nguzo ya mafanikio. Hukusukuma kujaribu mambo mapya na ustahimilivu kwenye changamoto. Utafiti kwenye chuo kikuu cha Melbourne, ulibaini kuwa watu wanaojiamini hulipwa ujira mkubwa zaidi na hupewa promotion zaidi kuliko wenzao wasiojiamini.
Kulala bila nguo kunaipa ngozi yako utulivu. Pale utulivu unapoongezeka kwenye mwili wako, vivyo hivyo hali ya kujiamini inaongezeka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni