Msanii wa hip hop aliyewai kufanya vizuri na Kundi la East Coast Team, King Crazy GK amesema kwa sasa hafanyi show chini ya Tsh milioni 30.
Rapper huyo amedai hawezekani msanii kutoka nje alipwe zaidi ya Tsh milioni 100 alafu msanii wa ndani alipwe chini ya milioni 30.
“Kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi lazima awe amejikamilisha,” GK alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Kwa sababu ukiangalia wasanii wanaotoka nje ya Tanzania wakija huku wanalipwa hadi milioni 100, lakini sisi wa ndani hela inakuwa ndogo naamini tunaweza na muziki tunaofanya ni mzuri media zikiendelea kusapoti naamini hata sisi tuna uwezo wa kulipwa hela hizo,”
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mzuri Pesa amesema kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya naye kazi lazima awe amejipanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni