burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

16 Sep 2016

Chemical afunguka sababu ya kuwashirikisha wasanii wasiofahamika

Rapper wa kike Bongo mwenye swagga za hatari, Chemical amefunguka sababu ya kuwashirikisha wasanii wasiojulikana japo tayari ameshakuwa na connection ya kuweza kufanya kazi na wasanii wakubwa Bongo.
chemical
Chemical ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anataka asimame mwenyewe ili hata akimshirikisha msanii mkubwa asionekane amebebwa.
“Nawashirikisha wasanii wasiokuwa na majina si kwa sababu sina connection, hapana. Mimi napenda kitu kizuri na mtu anayefanya vizuri napenda kufanya naye kazi, lakini kitu kingine kikubwa zaidi huwa sipendi kumfuata mtu complete nifanye naye collabo aanze kunishangaa,” amesema Chemical.
“Najaribu kwanza kusimama mimi mwenyewe hata mwisho wa siku nikitaka collabo na staa awe anajua kabisa Chemical anaweza kwa kuwa muda mwingine ukimfuata staa anajaribu kupreview kwanza ili amjue Chemical vizuri ndio ufanya naye kazi,” ameongeza.
“Ndio maana nataka nisimame mwenyewe at the end of the day hata nikimfuata staa yeyote inakuwa ni rahisi kwa sababu anamjua Chemical ni nani sitaki kuonekana kama nataka kubebwa.”
Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Am Sorry Mama’ aliomshirikisha Centano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni