burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Okt 2016

Barakah The Prince: Nay wa Mitego hana akili, ni mp*mbavu, ni rapper anayeungaunga

Image result for nay wa mitego

Barakah The Prince ametema cheche – tena cheche za moto mkali.Baada ya Nay wa Mitego kudai kuwa muimbaji huyo wa ‘Nisamehe’ na Stan Bakora ni watoto na kwamba huenda wanatafuta kiki, ameibuka na kudai kuwa rapper huyo hana akili na mp*mbavu.
“Nay hana akili, yaani Nay wa Mitego ni mp*mbavu tu,” Barakah alimwambia mtangazaji wa kipindi cha Mdundo Bando cha Lake FM, JR Junior.
“Yeye ndio anaishi kwa makiki ndio maana mpaka alifungiwa kwa kupiga madada za watu picha za uchi, sio mwanamuziki mzuri,” alisisitiza msanii huyo.
“Nay wa Mitego ni rapper anayeungaunga, yaani huwezi kumweka miongoni kwa rappers wakali Bongo, huwezi kunitajia Nay wa Mitego nikakuambia kwamba ni rapper mkali. Kwahiyo naye akija akaongea shit about me yaani nitamshangaa.”
Msikilize zaidi Barakah hapo juu akiporomosha mabomu!

Jiunge na g.loveTZ.com sasa

Gusa HAPA kwa kumjua zaidi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni