burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Okt 2016

Collabo nyingi za Afrika na Marekani zinawafaidisha Wamarekani kuliko sisi – Vanessa Mdee

Image result for Vanessa Mdee

Usitarajie kabisa kusikia collabo ya Vanessa Mdee na msanii wa Marekani siku za hivi karibuni.Muimbaji huyo wa Juu, amesema muda wa kufanya hivyo kwake bado haujafika. “Nadhani nitawafaidisha zaidi wao zaidi ya wao kunifaidisha mimi,” Vanessa alisema Jumatano hii kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Because hawatafanya promo ya wimbo wetu Marekani but mimi nitafanya promo ya wimbo wao huku Afrika,” aliongeza. “So I want to get to a point where kama vile Wizkid alivyofanya One Dance imewafaidisha wote wawili. So bado hatujafikia hatua ya kusema kwamba now I am going to work with, na tutafanya equal promo, haipo! What is it for kama wote hamfikii mashabiki wa wenzako, it doesn’t make any sense.”
Vanessa alitolea mfano wimbo wa Davido aliomshirikisha Meek Mill ‘Fans Mi’ ambao msanii huyo wa Marekani hakuwahi kusema chochote.
“Meek hata kupost kicover hajapost, so what is it for na amelipwa hela nyingi sana, I don’t know if we can do that,” alisisitiza.
Watangazaji wa kipindi hicho nao waliyaunga mkono mawazo ya Vanessa.

Jiunge na g.loveTZ.com sasa

Gusa HAPA kwa kumjua zaidi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni