burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

10 Okt 2016

Snura asema wimbo ‘Chura’ ni wimbo wake wa kwanza kumtambulisha vizuri kimataifa

Msanii wa muziki Snura Mushi amesema anauheshimu sana wimbo wake ‘Chura’ kwa kuwa wimbo huo ndio wimbo wake wa kwanza kumtambulisha vizuri kimataifa.
snura
 siku chache baada ya wimbo huo kuruhusiwa kuchezwa katika vituo vya redio na runinga baada ya ule wa mwanzo kufungiwa, Snura alisema wimbo huo umeweza kumtambulisha vizuri katika mataifa mbalimbali duniani.
“Nashukuru Mungu ‘Chura’ amerudi, tena vizuri, kwa sababu nilikuwa naulizwa sana kwenye majukwaa mbalimbali,” alisema Snura “Huu ndiyo wimbo wangu ulioanza kujulikana na kunitambulisha vizuri kimataifa, hivi karibuni nilikuwa na tour za kimatifa mashabiki wengi wa nje wamtaka ‘Chura’. Kwa hiyo naweza kusema wimbo wa Chura umebeba historia kubwa katika muziki wangu,”
Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni