burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Okt 2016

Siwezi kushoot video nje kwa gharama kubwa wakati nachoingiza ni kidogo – Stamina

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro, Stamina amesema hawezi kwenda kushoot video nje kwa pesa nyingi wakati anaingiza pesa kidogo katika muziki wake.
Stamina2
“Muziki ni biashara na biashara kinachoingia ndicho unatakiwa ukitoe,” alisema Stamina “Huwezi ukawa kwa mwezi unaingiza milioni 2 halafu ndani ya mwezi unatumia milioni 30. Hiyo ni hasara, namaanisha kinachoingia kiwe sawa sawa nakinachotoka,”
Aliongeza, “Lakini mimi sasa hivi naona muda bado kutokana na bajeti, kwa sababu mimi ni msanii ambaye toka naanza muziki sijawahi kuwa na manager, toka naanza muziki najisimamia mwenyewe. Tunapata hela za shows lakini tuna majukumu mengi, mimi natakiwa kula, kuvaa, nilipe kodi bado kuna familia zinakuangalia. Labda kama kungekuwa na mtu nyuma ambaye angekuwa anatoa hizo pesa, lakini katika kila pesa ninayoipata inamahesabu mengi na inanifanya nishindwe kutoa pesa nyingi kwenye vitu kama hivyo,”
Pia rapper huyo amesema kuna baadhi ya watu walijitokeza kumsimamia lakini baada ya kukaa nao kwa muda mfupi akaachana nao baada ya kuona hawawezi kumpatia vitu anavyotaka.
“Kuna watu walijitokeza lakini tulishindwana, unajua hapa nilipo tayari nimeshafikisha muziki wangu sehemu fulani, unavyokuja kunisimamia sio kama mtu ambaye una msimamia msanii mchanga, kwa hiyo uje na mipango iliyokuwa thabiti. Hapa katikati kuna watu walikuja, siwezi kuwachoresha lakini ndani ya mwezi mmoja tukashindwana, kwa sababu mahitaji yangu nayotoka wakawa hawawezi kuyatimiza, tukashindwana, kwa hiyo kusimamiwa sikatai lakini natama mipango,”
Rapper huyo anajipanga kuachia albamu yake mpya Disemba mwaka huu baada ya albamu yake iliyopita, ‘Mt Uluguru’ kufanya vizuri kwa kuuza zaidi ya nakala 9,000.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni