burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Okt 2016

Lover Boy imeonyesha ni jinsi gani nimeweza kubadilika na kufanya kitu kizuri- Barnaba

barnaba


Mkali wa wimbo ‘Lover Boy’ Barnaba Classic amefunguka kwa kusema kuwa kubadilika kwake kwenye wimbo ‘Lover Boy’ ndio kitu pekee kilichoufanya wimbo huo ukafanya vizuri.Barnaba amesema wimbo huo kila kukicha unaendelea kufanya vizuri zaidi hali ambayo inamfanya aendelee kuufanyia promo ili ufike mbali zaidi.
“Kusema kweli ‘Lover Boy’ umekuwa wimbo mkubwa sana, kila kukicha naendelea kupokea naoni tofauti tofauti, kwa hiyo ni jambo la kumshukuru Mungu,” alisema Barnaba “Mashabiki wamependa jinsi nilivyobadilika kwenye ‘Lover Boy’ na kufanya kitu tofauti na nyimbo zangu zilizopita, kwa hiyo mimi sina chakuzungumza zaidi ya kuandaa kazi nzuri zaidi, nimeonyesha ufundi wangu kwenye uandishi na watu wamependa,”
Muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki wa ‘High Table Sound’ amesema atahakikisha anaufanyia zaidi wimbo huo promo ili kuufanya wimbo huo kufika mbali zaidi.

Jiunge na g.loveTZ.com sasa

Gusa HAPA kwa kumjua zaidi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni