burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Okt 2016

Mandojo na Domokaya kushoot video nje ya nchi ili kukabiliana na ushindani uliopo

Wasanii wa muziki waliowahi kufanya vizuri na wimbo ‘Nikupe Nini’, Mandojo na Domokaya wamesema wapo tayari kwa sasa kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kushoot video za nyimbo zao.
Mandojo
Wawili hao walisema ili kushindana na wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye game ni lazima kufanya kazi nzuri zaidi yao.
“Muziki ni biashara na game sasa hivi kusema kweli imechangamka, kwa hiyo hata sisi tupo tayari kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kushoot video,” Mandojo alikiambia kipindi cha On Point ya Clouds FM.
Pia wawili hao wamemtaja AliKiba na Diamond kuwa ni miongoni mwa wasanii ambao wanatamani kufanya nao kazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni