burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Okt 2016

Lord Eyez awarushia mtego Weusi, adai wamekuwa wakimminya

Weusi inaundwa na members watano, Joh Makini, G-Nako, Nick wa Pili, Lord Eyez na Bonta, lakini ni watatu ndio ambao huonekana zaidi.
cufc7gcwcaa7q8t
Lord Eyez (wa pili kulia) akiwa na crew ya XXL – B12, Mami Baby, Kennedy The Remedy na DJ Sinyorita
Miezi kadhaa iliyopita, Nick amekuwa akidai kuwa Lord amesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya kundi/kampuni hiyo.
Na sasa Lord ameibuka kwa kudai kuwa licha ya kuendelea kuwa na ushkaji na members hao watatu, kuna sehemu wanamminya.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Alhamis hii, Lord alisema akiwa mmoja wa waasisi wa kampuni hiyo, atakuja kueleza zaidi ya ndani yanayoendelea.
Anadai kuwa makubaliano ya kampuni hiyo ni kuwa member asiyepanda kutumbuiza hapati mkate wake, na yeye kwakuwa hahusiki sana na show zao amekuwa akiambulia patupu. “Kimuziki uhusiano wetu na Weusi mimi Joh Makini Gnako na Nick wa Pili tupo vizuri ila kwenye maslahi kuna kuminywa sana,” alisema.
Rapper huyo aliyewahi kung’ara enzi za Nako 2 Nako, alipanda kwenye show ya Fiesta jijini Arusha baada ya kualikwa na Barakah Da Prince. “Nilipanda na Baraka Da Prince kwasababu Baraka ndiye aliyeona umuhimu wangu mimi kuwepo Arusha. Alinifata nikiwa bado sijapokea simu ya mtu yeyote,” alisema.
“Kuna watu waliingilia kati kuweka zengwe nisitumbuize na Barakah lakini nilifanikisha kwa kishindo.”
December mwaka jana hata hivyo alipohojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Lord Eyez alikuwa na hadithi tofauti.
Alisema bado yupo fresh na kundi hilo na anatarajia kuachia ngoma mbili, ‘Hardcore’ na ‘Shida Mpya’ alizomshirikisha member wa kundi hilo G -Nako.
“Lord Eyez bado nipo na nilikuwa na napikapika vitu,” alisema. “Juzi kati nilikuwa na G-Nako tukiwakilisha Weusi kampuni na sasa hivi tayari tumeandaa kazi mbili, moja inaitwa Hardcore na nyingine Shida Mpya,” aliongeza.
“Kwahiyo nawaambia mashabiki wangu wakae mkao wa kula, nataka nifunge mwaka halafu nifungue kwa kasi kwa sababu nataka mwaka 2016 uwe mwaka wangu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni