burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

14 Okt 2016

Diamond atoa zaidi ya Tsh milioni 40 kununua mixer kubwa ya ‘Wasafi Records’

diamond
Mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya ‘Wasafi Records’ ambayo tayari imeshaanza kushafanya hits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chart mbalimbali za muziki nchini.
Muimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba na kumueleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.
“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwa hatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe order watutengenezee,” Diamond alimwambia Waziri January. “Zingekuwa ni zile ndogo ndogo wangenipa lakini kwa sababu hii ni kubwa sana lazima utoe order, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu,”
Pia Waziri January Makamba alimsifia producer wa ‘Wasafi Record’ Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond ‘Salome’ ambao kwa sasa unafanya vizuri.

Jiunge na g.loveTZ.com sasa

Gusa HAPA kwa kumjua zaidi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni