burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

12 Jan 2017

Marco Chali yupo chimbo kuandaa album yake


Marco Chali ameadimika kwa kiasi kikubwa si tu katika mzunguko wa nyimbo mpya, bali hata yeye mwenyewe haonekani kabisa siku hizi.
Kunani? Mara ya mwisho nilimpigia simu kutaka kujua nini anachokiandaa, alikataa katakata kuongea chochote akidai kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika.

Na sasa huenda tukawa tumepata jibu la kwanini amekuwa kimya na nini anachokifanya. Rapper Izzo Bizness ndiye aliyetoa siri kwa kudai kuwa producer huyo wa MJ Records anaanda album yake.

“Marco alinipigia simu, wiki kama tatu zilizopita na aliniambia anafanya album yake so kuna track moja amenipa, kwahiyo aliniambia nijipange, so project na Marco very soon,” Izzo alimuambia Lil Ommy wa Times FM kupitia show yake ya The Playlist.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni