burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

31 Jan 2017

Mrisho Mpoto awataka wasanii kuwa kitu kimoja ‘tusiwe wasanii wa bila hit song maisha hayaendi’


Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewataka wasanii kuondoa makundi yaliyopo kwenye muziki na kuanza kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa wengi.
Muimbaji huyo amedai kila msanii anafanya kazi kivyake hali ambayo inawanyima zaidi wasanii fursa za kibiashara.

“Kwa muda mrefu sasa wasanii wa Tanzania wamekua wakifanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi, lakini kila mtu anacheza karata yake kivyake kutokana na network na nguvu yake,” Mpoto alitoa taarifa hiyo Instagram. “Nadhani sasa wakati umefika kuondoa tofauti zetu, makundi, tukawa team moja tukae tuone tunawezaje kusaidiana kwenye nyanja za kibiashara,”

Aliongeza, “Kuwa kama wasanii wa Taifa la Tanzania wenye muelekeo mmoja bila kuingilia fani ya mtu wala maisha binafsi, Wazo langu tusitawanyike ikawa kila mtu anaenda kivyake, ukiotea hit basi ndiyo unapata hela, najaribu tu kuwaza kwa sauti kama wazo lina mashiko, #teamtanzania,”

Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao wanapiga deal nyingi nje ya muziki ukiachia mbali deal za ubalozi za makumpuni mbalimbali alizopewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni