burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Jan 2017

Mchekeshaji Masele Chapombe afunga ndoa


Msanii wa vichekesho aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia Kundi la Vituko Shoo, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’ weekend hii ameaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Specioza Malick iliyofungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam.
Desemba 23, 2016 Masele na Specioza walifanya send-off Moshi, Kilimanjaro, nyumbani kwa mwanamke huyo.
Muigizaji amekuwa msanii wa kwanza kufunga ndoa ndani ya mwaka 2017.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni