burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

5 Jan 2017

Young Killer asikitishwa na taarifa za Young Dee kurudi kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya


Msanii wa muziki wa hip hop, Young Killer Msodoki ni mmoja kati ya wasanii walioshtushwa na taarifa ya rapper mwenzake Young Dee kurudi kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya.

Meneja wa rapper huyo aitwaye Max alionekana akilalamika kupitia mtandao ya kijamii kueleza jinsi rapper huyo alivyorudi katika janga hilo.

Akiongea na  rapper Young Killer amedai yeye ni mmoja kati ya watu waliopokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

“Mimi nachoweza kumwambia ajitambue, akumbuke dhamana aliyopewa na Mungu ya kuwa kioo cha jamii anatakiwa kuitumia vizuri,” alisema Young Killer. “Waswahili wanasema Kijua ni hiki usipo uanika sasa, utautwanga mbichi, sasa kazi kwake,”

Pia rapper huyo amedai wasanii wengi wanashindwa kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya kwa kuwa wao wenyewe hawataki ila wanalizishwa na watu.

“Kusema kweli wengi wanashindwa kuacha Madawa kwa sababu mioyo yao haipo tayari kuachana na hali hiyo, sisi wasanii au mashabiki tunawalazimisha kufanya hivyo na wao wanafanya hivyo ili kuwadanganya mashabiki lakini ndani ya nafsi zao wanajua wanachokifa,”

Katika hatua nyingine rapper huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa kazi zake mpya ambazo amedai sitatoka siku za karibuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni