burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Jan 2017

Vanessa Mdee azitaja sababu 4 za kwanini hana mpango wa kumshirikisha msanii wa Marekani kwa sasa

Image result for vanessa mdee niroge
Wakati anaanza muziki, Vanessa Mdee kupitia kazi yake ya utangazaji katika kituo cha runinga cha MTV Base, alikuwa ameshakutana na wasanii wenye majina makubwa Marekani.
Kwa kawaida, mtu mwingine angetumia advantage hiyo kutaka collabo nao, lakini si kwa Vee Money. Hadi leo akiwa na miaka minne tangu aanze muziki rasmi, Vanessa haoneshi kuwa na haraka ya kuwashirikisha wasanii wa Marekani, kwanini?

“Namba moja, kila kitu kina wakati wake, two, unaweza ukafanya collabo na msanii wa kimataifa na muda wake haujafika, haitafikia pale unapolenga ifike,” ameiambia Bongo5.

“Three, msanii wa Marekani au wa nje ambaye ana mileage kubwa kukushinda wewe, hawezi hata siku moja kukupromote na maana ya collaborations ni kuleta audience mbili tofauti zije pamoja kutengeneza nguvu kubwa zaidi,” ameongeza.

Vee amedai kuwa collabo na msanii mkubwa wa Marekani inaweza kufanikiwa iwapo tu kutakuwepo na ushkaji mkubwa kati yao na tena wa muda mrefu na awe anajua hustle ya msanii huyo na anatamani afike sehemu.

“Halafu hizi collabo nyingi kuna kulipana na nini, it doesn’t make sense. And watu wanakuja Afrika, hiyo ni pointi ya nne, so If you the baddest in Africa, baddest in Tanzania, watakujua tu so I am not in a rush kutengeneza nyimbo ambayo haitaenda kufikia the top of the charts. I am in a rush to create a brand so big that wao wenyewe watakuja kunitafuta,” amesisitiza Vanessa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni