burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

31 Jan 2017

Tunda Man aweka wazi ratiba ya muziki wake ndani ya mwaka 2017


Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amedai tayari ameshafanya maandalizi ya kutosha kwajili ya mashabiki wa muziki wake ndani ya mwaka 2017.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Tunda Man amedai ndani ya mwaka huu ataachia nyimbo 5 pamoja na video zake.

“Namshukuru Mungu mwaka umenza vizuri na ratiba yangu ya mwaka au kalenda yangu imepangika vizuri. Nitaachia nyimbo tano pamoja na video zake, sitaki mwaka huu kutoa ngoma chache kwa sababu muziki wa sasa umebadilika mashabiki wanataka kazi nyingi zaidi,” alisema Tunda Man.

Aliongeza, “Kwa hiyo kazi zipo nyingi, kuna ngoma nimefanya na Yamoto Band, kuna wimbo nimefanya na Jaguar wa Kenya, yaani kuna kazi nyingi Mungu akitujalia ngoma tano zitatoka mwaka huu,”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Debe Tupu’ ambao aliuachia January mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni