burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

Achana na ‘Sinaga Swagger’, naweza kubadili matokeo muda wowote – Young Killer


Rapa Young Killer Msodoki, baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Sinaga Swagger’ amedai hataki mashabiki wajue atakuja vipi katika project yake inayofuata.

Wimbo uliopita wa rapa huyo ulizua gumzo mtaani na katika vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuwachana baadhi ya wasanii wenzake.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Young Killer amedai tayari ameandaa kazi nyingi kwa ajili ya ujio wake mpya lakini hataki mashabiki wajue kama ataendelea na ngoma za kuwachana wasanii wenzake au la.

“Baada ya ‘Sinaga Swagger’ kuwachana wale wana, kiukweli kabisa nina project nyingi kali na muda wowote au saa yoyote naweza kubadilisha matokeo kwa sababu kuna nyimbo nyingi ndani kali ambazo hata sijajua ninazitoa lini au saa ngapi. So Watanzania wategemee vitu vizuri na kwa mtindo wowote,” alisema Young Killer Msodoki.

Rapa huyo ambaye ni zao la Serengeti Super Nyota, ni mmoja kati ya marapa vijana ambao wanafanya vizuri kwa sasa kwenye game ya muziki wa hip hop.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni