burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

Sportpesa yatua bongo kwa kishindo, Yanga na Simba SC kutajirishwa


Hatimaye kampuni ya kubashiri matokeo, ya Sportpesa ya nchini Kenya, rasmi imetua jijini Dar kuidhamini klabu kongwe ya Yanga. Kampuni hiyo itawadhamini Yanga na Simba baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyokuwa yakifanyika kati ya klabu hiyo na uongozi wa Sportpesa.


Kikosi cha klabu ya Yanga.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja nchini Kenya,, kampuni hiyo imetua nchini kwa ajili ya kuzindua matawi yake Tanzania na uzinduzi unatarajiwa kufanyika Mei 9, mwaka huu kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, iliyopo Kivukoni jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa pamoja na kuzindua matawi, pia Sportpesa itapata nafasi ya kukutana na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo ya mwisho kabla ya kuingia mkataba.

“Kwa heshima na taadhima mnaalikwa katika uzinduzi wa Sportpesa Tanzania Jumanne ya Mei 9, 2017 katika Ukumbi wa Kibo Ballroom kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Barabara ya Kivukoni,” ilisomeka taarifa kutoka katika mtandao huo.


Kikosi cha klabu ya Simba Sc.

Sportpesa tayari ni wadhamini wa Hull City inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Gor Mahia, AFC Leopards zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, pamoja na klabu nyingine kadhaa katika soka la Kenya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni