burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

Nikki wa Pili aja na zawadi kwa mashabiki wake


Image result for NIKKI WA PILI
Msanii wa Pili kutoka kundi la Weusi ameweka wazi kuwa wiki ijayo atatoa wimbo mpya. Hii ni baada ya kimya cha muda mrefu tangu alipotoa wimbo wa ‘Sweet Mangi’ kisha kufuatiwa na ‘project’ nyingine za kundi.

Nikki amedhibitisha ujio wake huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter. “New Muzik…. next week…… mwendelezo mwingie wa mapinduzi ya uandishi na flow…..,” aliandika Nikki.



Katika kundi la Weusi ambalo linaundwa na yeye pamoja na Joh Makini, Bonta na G Nako, Nikki ndiye msanii pekee ambaye mwaka huu hajatoa wimbo wake binafsi zaidi ya kushiriki kwenye wimbo wa kundi ‘Yakulevya’.

Joh Makini alianza kwa kutoa ‘Waya’, kisha G Nako akatoa ‘Go Low’ aliyoshiriakana na Jux. Bonta ameshatoa wimbo uitwao ‘Zero’ aliyomshirikisha Baraka the Prince, sasa ni zamu ya Nikki wa Pili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni