burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mei 2017

BIRDMAN NA LIL WAYNE WAZUA MASWALI NA KUWAACHA MASHABIKI MIDOMO WAZI


Rapa anayefanya kazi chini ya lebo ya muziki inayomilikiwa na Jay Z ya Roc Nation Records, Lil Wayne amefanya tukio ambalo wengi waliomfatilia hawakutegemea kwa kipindi hiki cha kutoelewana kibiashara na lebo yake ya zamani ya Cash Money Records kabla kuingia rasmi katika mkataba mpya wa kiabishara na Rock Nation.

Katika Rolling Loud festival ilayoendelea huko Miami Florida rapa Lil Wayne aliwashangaza mashabiki waliokuwa na taarifa za kuwepo kwa bifu nzito kati yake na mfanyabishara na rapa nayemiliki lebo ya Cash Money Records baada ya kukubali kupiga picha na watoto wawili wa Birdman Bryan Jr. na Bria.

Aidha zengwe hilo haikuishia hapo kwenye kupiga picha pekee kwakuwa mara baada ya picha hizo za kumbukumbu za watoto wa mmiliki wa lebo ya Cash Money Records Birdman na Lil Wayne picha liliendelea kupitia akaunti ya Instagram ya Birdman kwakuwa alizipost kitendo ambacho kiliacha maswali na majibu ya kuwa inawzekana hakuna tatizo kati yao kwasasa.







Hata hivyo Lil Wayne tangu kuingia mkataba wake mpya na Rock Nation ameonekana katika kazi mpya ya DJ Khaled ya I’m the One iliyowashirikisha Justin Bieber, Quavo na Chance the Rapper inayoenakana kuwa na mapokezi makubwa sana kwakuwa imefikisha watazamaji zaidi ya milioni 78 ndani ya wiki moja pekee katika mtandao wa Youtube.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni