burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mei 2017

EXCLUSIVE: QUICK ROCKA AFUNGUKA KUHUSU UMAARUFU WA BULLET, KUNDI LA ROCKAZ, KAJALA, SWITCH RECS NA KUPISHANA NA NAHREEL


Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Quick Rocka aligeuka kuwa jina maarufu kwenye Hip Hop ya Tanzania, thanks kwa hit single yake, Bullet. Wimbo huo ulimpa sifa ya kuwa rapper anayerap kwa kasi zaidi katika muziki wa Bongo – kama jina lake.

Quick anasema wimbo huo ulikuja katika kipindi ambacho alikuwa amejiandaa nusu, na nusu nyingine umaarufu ulimwijia kama upepo wa jangwani.
Maisha yalibadilika kwa kasi na kujikuta akiwa busy kila wikiendi kwa show ambazo hazikuwa zikikoma.

“Every weekend I was booked,” anasema Quick nilipozungumza naye kwenye kipindi changu, Chill na Sky: Reloaded. “Na kuna time nilikuwa nazunguka sana mpaka nachoka, mpaka sometimes kuna show nazibonyeza, yaani mwili unagoma. Bullet ilinifanya mtu ambaye niko leo,” amesema.

Pamoja na mafanikio ya mwanzo mwanzo akiwa mwenyewe, Quick alikuwa kwenye kundi la hip hop lililowahi kutamba sana, Rockaz. Kundi hilo liliundwa na members wanne, yeye, Chief Rocka, Dau Rocka na Mo Rocka. Anasema yeye na Chief walikuwa wakifahamiana kitambo kwakuwa ni mtoto wa dada yake. Ni Chief ndiye aliyewaleta pamoja kwakuwa alikuwa akifahamiana na Dau na Mo. Baada ya kundi lao kuundwa, lilibatizwa jina la MGT Fellaz kabla ya mtu mmoja aitwaye Kabwe kuwapa jina Rockaz kutokana na uwezo wao kuchana, jina ambalo lilipita na kila mmoja kuwa sehemu ya jina lake.

Ni Mo Rocka ndiye aliyewaunganisha members wenzake kwa Lamar aliyekuwa amesharekodi naye ngoma zake za solo ukiwemo Ninashine. Quick anasema baada ya siku kama tatu baada ya kutambulishwa walifanya kazi yao ya kwanza ya kundi, Rockaz Anthem iliyotamba vikali redioni. Hata hivyo kundi hilo halikuweza kudumu kwa miaka mingi.

“Hatukuwa tayari,” Quick anasema kuhusiana na sababu za kuvunjika kwa kundi lao. “We had this chemistry na tulikuwa tunafanya muziki as a hobby, as fun, tulikuwa tunaenjoy watu wanavyosikia, watu wanavyovibe, vitu kama hivyo. Kila tatizo huanza pale pesa inapoanza kuingia, hapo ndio kunakuwaga na mipishano. Then by the time mimi nikawa niko signed under MJ, kwahiyo mimi J alivyonicheki tu nikawaambia ‘there is this on the table, it’s an opportunity.’ Wengine walikubali, wengine walikataa, so pale kwenye kukubali kataa ndo kundi likasplit,” anakumbushia rapper huyo.

Quick amesema juhudi za kulirudisha tena kundi baada ya miaka kadhaa baadaye zilifanyika lakini hazikuzaa matunda. Amesema sababu ni kushindwa kutumia muda mwingi pamoja ili kutengeneza chemistry mpya.

“Kundi lilipovunjika, Chief alisafiri akaenda China kusoma for five years. Baada ya three years aliporudi ndio tukasema let’s bring it back, tukajaribu the chemistry wasn’t there. Tulijaribu sana, unajua tunachekiana tunaenda studio it’s trash so hauwezi ukalazimisha.”

Baada ya kukaa kwa muda MJ Records na kisha mkataba kuisha, alianza kufanya kazi na Manecky ambaye alitengeneza naye wimbo My Baby aliomshirikisha marehemu Ngwair. Uhuru wa kurekodi ngoma muda wowote aliokuwa nao MJ ulipotea.

“Kipindi hicho nafanya kazi na Manecky, nilianza kununua vyombo taratibu, ili kuepukana na hiyo – sipendagi kuombaomba, ndivyo nilivyo,” anaeleza Quick. “So nikawa nanunua vyombo taratibu mpaka nikawa complete navyo vyote lakini bado nafanya kazi kwa Manecky. Then there is this day nilikuwa naumwa, Manecky na Tudd wakaja kunicheck home. Wameingia chumbani kwangu wakakuta nina maspika, mixer, everything wakasema ‘yaani wewe unaumwa halafu una studio ndani!’ nikasema ‘bado nataka nipige building fulani’ wakasema ‘hizi hizi, usitafute hela zingine, hizi zitakuletea hela ujenge studio, ufanye nini so you have to start with this.’ Walinipush sana kusema ukweli na I have to thank them Manecky na Tudd na nakumbuka kompyuta ya kwanza ya Switch alinipa Manecky.”

Rapper huyo ambaye hujiita Switcher, anasema baada ya kuifunga vizuri studio yake alimtafuta Nahreel ambaye alimkabidhi kiti cha uproducer kwenye studio yake, Switch Records.

Hata hivyo baada ya kufanya kazi kwa muda, Nahreel aliondoka kwenye studio hizo na kwenda kuanzisha zake, The Industry. Kuachana kwao hakukuwa kwa amani na hivyo wakajikuta wamekuwa maadui kwa muda. “[Nahreel] hakuniweka wazi kwamba kuna moja mbili. Ujue unapofanya kazi na mtu, hata kama unaondoka kwamba ‘oi, mimi nasepa’ kiroho safi, hamna mtu tunashikana cause hatujui leo yako, kesho yangu ikoje, wote tunatafuta so aliondoka kimya kimya tu,leo kaja studio, kesho hayupo tena, hicho ndio kitu kilinikera.”

Pamoja na hivyo, Quick na Nahreel sasa ni marafiki tena na anaona ulikuwa uamuzi wenye faida. “Tulifanya kazi Switch ikasikika, then he went away which is a good thing akaenda kuintroduce The Industry ambayo sasa hivi ni label kubwa, studio nzuri, inafanya kazi.”

Pia hilo lilikuwa somo kwake kuwa hapaswi kumtegemea mtu katika kuhakikisha kuwa Switch Records inasonga mbele. Baadaye alikuja kumpata Luffa aliyeunganishwa na ndugu yake, japo mwanzoni hakuwa mzuri kama alivyo sasa na alipewa ujuzi zaidi na lundo la maproducer wazoefu walio karibu na Quick wakiwemo Bano, Dupy, Bob Manecky na Chizan Brain.

Kwa upande wa uhusiano Quick amewahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na Kajala, kitu ambacho amekuwa akikikana hadi sasa licha ya kuwahi kujipost wakibusiana. “Hatukuwahi kuwa wapenzi,” anasema.

“Zile nyingi ukiangalia ni vitu ambavyo mtu mwingine alikuwa anashoot, ni sehemu ambapo tulikuwa tunafanya movie, tunafanya hivi, vipisi vinakatwa. Kuna movie ilitoka ilikuwa inaitwa Wake Up na vipisi vingi vilivyokuwepo viliondolewa, I don’t know why,” ameongeza Quick kwa kicheko.
Kwa sasa anadai ameweka mapenzi pembeni na anajikita zaidi kwenye kazi.
“I am building something on this music industry, haya mambo mengine yatafuata baadaye tukishakuwa na chapaa nyingi.”

Msimamo huo wa Quick haumaanishi kuwa hakuna warembo anaowakubali hasa wa nje. “Wapo wengi,” anasema kwa kicheko. “Mmoja ambaye nikimuona tu inakuwaga noma, kuna Keri Hilson na Ashanti. Ashanti nimewahi kuwa shabiki wake mkubwa sana, nilikuwa napenda sana anavyoimba, jinsi anavyojipresent na mpaka leo yupo kwenye form.”

Kwa upande wa mipango ya kuoa, Quick anasema, “Haipo kwenye ratiba yangu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni