burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mei 2017

BAADA YA UKIMNYA WA MUDA MREFU KUNDI LA WA MELODY CLASSIC LA RUDI KWA KASI YA AJABU

Image may contain: 2 people, text

Baada Ya Ukimya Wa Muda Mrefu Kutoka Kwa Kundi La Wa Melody Classic Pepeza Pepeza Linalowakilishwa Na Wasanii Machachari Kutoka Kilimanjaro Hapa Namzungumzia Jobfire Wa MeLody Pamoja Na Single Sally Wa Melody

Kila Mtu Alikuwa Akiongea Lake Huku Tukiwasikia Wengine Wakisema Kwamba Hawa Jamaa Wana Bifu Zito Baina Yao Na Watu Hawategemei Kabisa Kuwaona Wakifanya Kazi Pamoja. Hayo Ni Maneno Yaliyokuwa Yakitoka Kwa Wadau Wa Mziki Huku Wakiongeza Kwa Kusema Kwamba Bifu Kubwa Ya Wasanii Hawa Ilipelekea Kuvunjika Kabisa Kwa Kundi Lao Na Kila Mtu Kuamua Kufanya Kazi Zake Peke Yake Na Kwa Wakati Wake.

Ila Cha Kushangaza Sasa Ni Kwamba Hivi Karibuni Zilianza Kusikika Tetesi Kwa Mashabiki Hao Hao Wakisema Kwamba Wawili Hao Single Sally Na Jobfire Wa MeLody Wamepatana Na Kuna Taarifa Kwamba Wamefanya Kazi Ya Pamoja Katika Studio Ya Defatality Music Chini Ya Mkono Wa Producer Mkali Messen Selector Tz. Baada Ya Uchunguzi Wa Kina Blog Yetu Imegundua Ukweli Na Kuthibitisha Taarifa Hizi Kwamba Ni Kweli Hawa Jamaa Wamepatana Na Soon Wanakuja Na Ngoma Mpya  Inayoitwa #CHARAMILLA.

Kumbe Hawa Jamaa Hawakuwahi Kugombana Ila Ni Mipangilio Yao Tu Ya Kazi Waliamua Kuwapa Brake Mashabiki Wao Ili Wakirudi Kama Kundi Wakate Kiu Kwa Mashabiki Na Hii Ndio Ilikuwa Plan Yao Kwa Mujibu Wa Majibu Yao Wote Wawili Baada Ya Kuongea Na Blog Yetu. Daaaaaah. Haya Sasa Pata Mziki Mzuri Soon Kutoka Kwa Wamelody Classic PepezaPepeza Cc// Singo Sally &  Jobfire Wa MeLody

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni