burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

HIVI NDIVYO CYRILL KAMIKAZE ALIVYONUSURIKA KUTEKWA PAMOJA NA AKINA ROMA


Kama si machale yake, Cyrill Kamikaze, naye angetekwa pamoja na akina Roma Mkatoliki kwenye tukio la utekaji lililotokea katika studio za Tongwe Records mwezi uliopita. Rapper huyo alifika katika studio hizo dakika 20 tu baada ya Roma na wenzie kuchukuliwa na watu wasiojulikana na kushikiliwa kwa takriban siku tatu.

“Mimi nilichelewa kama dakika 20 tu pale,” Kamikaze alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Na kisa cha kuchelewa nilikuwa namwelekeza mtu, yaani nimekaa kwenye simu namwelekeza mtu halafu kulikuwa na mvua fulani hivi inanyesha kwahiyo sikuweza kumove fast,” aliongeza.

Kamikaze alisema kuwa Tongwe ni sehemu ambayo huenda mara kibao hata wakati ambao hana kazi ya kurekodi. Rapper huyo amesema mwanzoni wakati ameambiwa kuhusu kuchukuliwa kwa Roma alidhani ni jambo la kawaida lakini kesho yake baada ya habari kuwa kubwa alipata uoga mkubwa.

“Sijatoka siku mbili,” alieleza. “Nikawa nahisi kuna masalia hivi wanataka wayamalizie sababu waliondoka hadi na house boy, kwahiyo iliniathiri sana nikaona hapa kutoka inawezakana nikarudiwa mimi unajua.”

Rapper huyo amesema kidogo hali za akina Roma zimeanza kurejea kawaida baada ya kuwa kwenye kipindi kigumu kimwili na kiakili baada ya kutekwa na kuteswa.

“Hata ukiwa ukiongea nao kwa mara ya kwanza unaona kabisa hawako sawa, lakini sasa hivi wako vizuri mentally soon tutawaona.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni