burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

5 Mei 2017

Nay wa Mitego amvuta Shamsa Ford kwenye ‘Wapo Tour’

Image result for Nay wa mitego na shamsa ford
Nani kakwambia wapenzi waliotengana au kuachana ni maadui?Sahau kabisa kuhusu hilo kwani Rapa Nay wa Mitego ameudhihirishia umma kwa kutangaza kuwa kwenye Tour yake ya muziki ‘Wapo Tour’ atasindikizwa na ex wake Shamsa Ford kwenye Special Appearance na pia atakuwa MC siku hiyo.

Nay wa Mitego amesema watu wengi huwa wanaamini mkiachana basi ndiyo mwisho wa urafiki lakini kumbe sio hivyo na ndiyo maana hata yeye ameamua kumleta Shamsa Ford kwenye Tour yake ya Wapo.

“Wapo Tour itakuwa ni ya Kipekee sana kwani itakuwa na list ya wasanii wawili watatu hivi wa kunisindikiza, lakini pia atakuwepo Shamsa Ford kwenye Special Appearance pia atakuwa kama MC kwa siku hiyo jukwaani,watu watarajie kuona burudani ya kipekee kabisa“Amesema Nay wa Mitego kwenye mahojiano yake na Bongo Five.

Nay wa Mitego na Shamsa Ford walishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma na baadae kuachana.

‘Wapo Tour’ itaanzia jijini Dar es Salaam tarehe 20 May Mwaka huu pale Dar Live,Mbagala na baadae kuelekea mikoani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni