burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mei 2017

NICKI MINAJ AWALIPIA MASHABIKI WAKE ADA ZA SHULE, WALIMTUMIA AKAUNTI ZAO ZA BENKI TWITTER


Nicki Minaj amezijaza akaunti za benki za mashabiki wenye bahati kwa fedha za kulipia ada zao za shule. Ilianza kama utani Twitter baada ya kuwataka mashabiki wake washiriki kwenye shindano analoliendesha ambalo linawapa nafasi kukutana naye.

Hata hivyo, shabiki mmoja aliichallenge kauli yake kuwa anaingiza fedha za kutosha kuwasafirisha mashabiki wake kokote duniani, kwa kumuomba awalipie ada zao za shule.



Nicki alichukua ushauri huo lakini akaweka kigezo kuwa atawalipia wale tu wanaofanya vizuri darasani. “Show me straight A’s that I can verify w/ur school and I’ll pay it. Who wants to join THAT contest?!?!??♀️ Dead serious. Shld I set it up,” alitweet.

Mashabiki kibao walijitokeza wakiwa na maombi ya kulipiwa ada, vitabu na vitu vingine vya darasani. Wengi walimuonesha screenshot za matokeo yao. Wale ambao walikuwa na A za kutosha, aliwaomba wamtumie DM akaunti zao za benki.

Na sasa TMZ imebaini kuwa Nicki Minaj hakuwa akiongea maneno tu. Imesema kuwwa tayari ameanza kuwatumia fedha mashabiki hao. TMZ imezungumza na baadhi ya mashabiki hao ambao wamethibitisha kuwa wamepokea fedha hizo ambapo mmoja amesema amepokea, $800 na mwingine $500.

Rapper huyo amesema atakuwa na awamu nyingine ya kutoa mpunga kwa mashabiki wake baada ya mwezi au miezi miwili.

“Ok u guys. It’s been fun. Let me make those payments tmrw then see if I have any money left?. I’ll do some more in a month or 2,” alitweet.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni