burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

23 Mei 2017

Riyama Ali kwa waigizaji wenzake – ‘Punguzeni kula bata’

Tokeo la picha la riyama ali bata
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Riyama Ali amewapa makavu waigizaji wenzake na kuwataka wapunguze kula bata kwani hata hizo pesa ndogo ndogo wanazozipata zinaweza kuwafanya waishi vizuri .

Riyama Ali ambaye alikuwa nchini Kenya kwa muda mrefu kwenye shughuli zake za kibiashara amesema kwamba, ni kweli Wasanii wa Bongo Movie wanakosa kiasi kikubwa cha pesa kutokana na kukosa haki miliki na ongezeko la kazi haramu.

“Tupigie haki miliki kelele wasanii sisi masikini lakini tunakazi nyingi nzuri leo hii haki miliki zetu hazipo mikononi mwetu,Stori zetu kazi zetu tusiwe bendera kufuata upepo uchungu tuufanye kwa vitendo sio kwa kushinikizwa na mtu“, Alisema Riyama Ali .

Hata hivyo amewachana pia wasanii wenzake kwa kusema wapunguze kula bata kwani pesa hizo wanazozipata ingawaje ni ndogo lakini zinatosha kuendesha maisha yao ya kila siku.

“Nawapenda sana wasanii wenzangu ila tukumbuke kuwa tunajukumu kwenye jamii,Jamii inatudai na tusile sana bata,Tunakula sana bata, punguzeni kula bata…..na ifike sehemu tukubali kuwa kuna mahali tuliteleza,tulilie sana haki miliki“, Alisema Riyama Ali kwenye mahojiano yake na EATV.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni