burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

5 Mei 2017

Diamond amkuna Mama Young Killer


Kitendo cha Diamond Platnumz kuamua kumshirikisha rapa Young Killer kwenye moja kati ya nyimbo zake zinazokuja kimemfurahisha mama mzazi wa rapa huyo.

Wiki chache zilizopita Diamond alisema kuna moja kati ya project zake ambazo zinakuja amemshikisha rapa huyo kijana huku akimmwagia sifa kwa uwezo mkubwa aliouonyesha kwenye project hiyo.

Akiongea na G.lovetz ijumaa hii, Young Killer amesema mama yake alifurahishwa sana na kitecho cha mkali hiyo wa ‘Marry You’ kutamka hadharani jinsi anavyoukubali muziki wa mtoto wake.

“Hiki kitendo kimenifanya nimuone Diamond Platnumz ni binadamu na ni mtu ambaye anastahili kuwepo sehemu ambayo yupo. Ni tukio ambalo limenitia faraja kiukweli hata mama yangu alivyosikia alifurahia sana na kumshukuru kwa kitendo ambacho amenifanyia,” alisema Young Killer.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni