burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

5 Mei 2017

‘Wapo’ ni baba lao katika nyimbo zangu zote – Nay wa Mitego


Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amedai wimbo wake ‘Wapo’ ni wimbo ambao umefanya vizuri kwa muda mchache kuliko nyimbo zake zote alizowahi kuziachia katika maisha yake ya muziki.

Akiongea na G.lovetz ijumaa hii, Nay wa Mitego amesema hata show zake zinajaza zaidi kuliko kipindi cha nyuma kutokana na wimbo huo.

“Nimeshatoa nyimbo zikawa kubwa, nimeshatoa nyimbo watu wakawa wanaimba, nimeshotoa nyimbo zikawa gumzo lakini ‘Wapo’ ni kiboko,” alisema Nay wa Mitego.

Aliongeza, “Ni wimbo ambao umefanya vizuri kila sehemu hata kwenye show mikoa yote niliyozunguka mambo yamekuwa ni mazuri sana. Kwahiyo naweza kuthubutu kusema Wapo ni kazi kubwa kuliko hata kazi zangu zote,”

Rapa huyo ambaye anatarajia kufanya show ya ‘Wapo Night’ mwezi huu katika ukumbi Dar Live jijini Dar es salaam, amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya remix ya wimbo huo.

Katika hatua nyingine, rapa huyo amewaka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumsupport msanii wake mpya B-Gway ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao ‘Sijachukua’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni