burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mei 2017

MEEK MILL AKUTANA NA ZAWADI YA MAPOKEZI KATIKA SIKU YA KUZALIWA KWAKE


Rapa na mmiliki wa lebo ya Dream Chasers Records ‘Meek Mill’ kufuatia kusherehekea siku ya mfanano wa kuzaliwa kwake siku ya jana alipata mapokezi ya kipekee huko visiwa vya Bahamas ambapo alipotua na kukanyaga ardhi kutoka katika ndege iliyomleta akiwa na timu yake alikutana na bendi ilimpokea kwa nyimbo shangwe na mizuka ya kumtakia mafaniko na siku njema ya kuzaliwa kwake.

Mapema siku ya jumamosi asubuhi Meek alisafiri kwa ajili ya kuianza wikiendi ya kusherehekea kuzaliwa kwake mbali na mapokezi ya bendi pia katika ufukwe wa visiwa hivyo alikutana na kibendela cha rangi ya machungwa kilichokuwa na ishara ya kuheshimu uwepo wake lililopambwa kwa maneno mawili ambayo ni DC maneno yanayosimama kama Dream Chasers jina ambalo linawakilisha lebo yake.

Hata hivyo mbali na kuitumia wikiendi hiyo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pia atafanya matamsha kadhaa yanayoendeleza ziara yake ndogo iliyopewa jina la MeekEND ambapo jana mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa rap duniani kote waliwapatia zawadi ya mixtape inayokwenda kwa jina la Meekend Music yenye ngoma tatu kama zawadi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni