burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

IZZO BIZNESS NA ABELA WAMETHIBITISHA KUWA WAPENZI KWENYE VIDEO HII MPYA?


Hayawi hayawi mwisho yamekuwa.. Kwa muda mrefu Izzo Bizness na member mwenzake wa kundi la The Amazing, Abela wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano. Hata hivyo, mara zote wamekuwa wakikanusha na kudai kuwa ni marafiki tu.

Huenda walitaka kutangaza uhusiano wao kwa njia inayofaa zaidi – kwenye wimbo. Wawili hao Ijumaa hii wameachia video ya wimbo wao mpya, Tumeoana ambayo inaonesha wakiuweka wazi uhusiano wao na tena kwa kuigiza wamefunga ndoa. Katika moja ya scenes mastaa hao wanaonekana wakibusiana kwa bashasha.

Video hiyo iliyoongozwa na Nick Dizzo, imetawaliwa kwa furaha kubwa katika nyuso zao na katika sehemu moja Izzo anaonekana akiwa amevalia suti nyeupe iliyomkaa vizuri na bi harusi, Abela akiwa ndani ya shela yake, ua mkononi. Kuna wakati wanaonekana wakicheza pamoja kwa madaha.

Tumeoana na wimbo mzuri sana uliotayarishwa na Abba huku ukiwa na vionjo vya kuvutia vilivyopendezeshwa na chorus tamu ya Abela.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni