burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

5 Mei 2017

‘Mchezo na Prisons tunauona kama fainali’ – Haruna Niyonzima

Image result for haruna niyonzima
Kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Klabu ya Yanga na Tanzania Prisons ya jijini Mbeya,Nahodha wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima amefunguka mengi jinsi anavyouchukulia mchezo huo dhidi ya kuwakabir maafande hao.

Image result for haruna niyonzima
Haruna Niyonzima wa Yanga akikimbilia mpira mwenye jezi ya Kijani.

Niyonzima amesema kwa sasa Klabu ya Yanga haipaswi kuangalia historia kwani mpira unabadilika kila kukicha na hivyo anaamini mechi hiyo itakuwa ni ngumu kwao na kuichukulia kama fainali.

“Mara kibao mimi sikubali historia Mimi siku zote kwenye mpira naangalia Present,so kitu kikubwa mimi naangalia ni mechi ya kesho,haijalishi tumewashinda michezo mingapi,Kitu kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha tunashinda kila mechi kwani kila mchezo una picha yake“Amesema Niyonzima na kuendelea kuuzungumzia mchezo wao kesho dhidi  Prinsons

“Mchezo na Prisons tunauona kama ni mchezo wa fainali kwani baada ya kupoteza mchezo wetu na Mbao tunahitaji kushinda ili kurudisha Morali kwa wachezaji na mashabiki wetu,Hivyo mchezo utakuwa mgumu kwetu so kwangu kwa kifupi mchezo wa kesho nauona ni mgumu kwani tunahitaji kushirikiana ili kushinda na kupata pointi 3“Amesema Niyonzima kwenye ukurasa wa Instagram wa Yanga.

Yanga kesho wanaikaribisha klabu ya Tanzania Prinsons uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwenye mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni