burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

21 Des 2016

Belle 9 afunguka ugumu uliopo wakati wa kushoot video nchini

Image result for Belle 9
Msanii wa muziki kutoka Vitamin Music Group Limited, Belle 9 amefunguka kuhusu ugumu uliopo wakati wa kushoot video nchini.
Akiongea na G.lovetz wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya ‘Give It To Me’ uliofanyika Jumamosi iliyopita, msanii huyo amesema, kuwa kuna ugumu sana wakati wa kutengeneza video nchini kwa kuwa kila kitu msanii ndio anatafuta.

“Nikiamka asubuhi nampigia simu video queen, nampigia director. Mimi nimekuwa sina muda mrefu sana kuwa na uongozi muda mwingi nimefanya game mwenyewe kwa hiyo nina hiyo experience ya vitu vingi unafanya mwenyewe. Even nilipokutana na uongozi video za bongo sisi wenyewe tulikuwa tunawatafuta watu,” amesema Belle.

Muimbaji huo ameongeza kuwa amependa utendaji kazi wa waongozaji wa video wa Afrika Kusini wapo makini sana na kazi zao kwani wao ndio huandaa kila kitu na msanii ndio anachagua vitu avitakavyo kwenye video yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni