burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

27 Des 2016

Nahreel ni miongoni mwa maproducer watakaonibadilisha – Chemical


Chemical amefunguka jinsi alivyojisikia baada ya kufanya kazi na Nahreel.
Mashabiki wamezoea kumuona Chemical akiachia kazi zake ambaozo zimetayarishwa na Maximizer lakini kwenye project mpya ya ‘Hola Hola’ imekuwa ya kwanza kumsikia rapper huyo akifanya na producer mwingine.

Akiongea na g.lovetz, Chemical amesema, “Nilifurahi kufanya kazi na Nahreel kwa sababu ni mtu ambaye nilikuwa natamani kufanya naye ngoma, ukiachana na hiyo ‘Hola Hola’ nilikuwa natamani sana kufanya naye ngoma yangu kama mimi.”

“Baada ya hiyo ‘ hola Hola’ nahisi kuna project yoyote nyingine inaweza ikatokea nikafanya na Nahreel na nitashukuru na nitapenda sana kwa sababu nahisi atakuwa ni miongoni mwa maproducer watakaweza kumbadilisha Chemical watu wakasikia ladha nyingine,” ameongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni