burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

21 Des 2016

Kuna watu wananikwaza, tusiwe tunaongea tu kuna wakati midomo inaumba – Mkubwa Fela

Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe ambaye pia ni diwani wa kata ya Kilungule Said Fella au Mkubwa Fella, amewataka watu kutambua mchango wake kabla hajafa badala ya kuponda jitihada zake huku akiwataka watu kuacha kuongea vitu wasivyovijua.

Fella ambaye pia ni boss wa Kundi la muziki la Yamoto Band, amesema watu wamekuwa wanaongoza kumsema vibaya badala ya kumsifia na kumpongeza, kwani kazi anayoifanya ni kubwa.

“Halafu kuna watu wanasemaga Said Fella sijui kawafukuza Yamoto, leo Yamoto wapo ndani humu,” Fella alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio “Nimekuja kukata midomo domo, kwa sababu tusiwe tunaongea tu inafika wakati ukweli midomo inaumba, Mkubwa na Wanawe ina watoto 102, kwa hiyo fella anatengeneza vingi, kuna watu wananikwaza, inatakiwa hata siku moja na mimi nipewe certificate ya kusaidia mtaa, kila siku wananibomoa wananibomoa, nisifieni kabla sijafa ninachokifanya hiki”,

Pia Mkubwa Fella alisema anayajua madai kuwa amewadhulumu Yamoto band, lakini ukweli ni kwamba vijana hao mpaka sasa kila mmoja ana nyumba yake, kitu ambacho kimetokana na juhudi zake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni