burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

23 Des 2016

Black Rhino awachana wasanii wanaotegemea kiki kwenye muziki


Rapper Black Rhino amewachana wasanii wanaotegemea kiki kwenye muziki wa Bongo Fleva ili wafanye vizuri.
Black amedai kuwa wasanii wengi wa kipindi hiki wamekuwa wakitegemea sana kiki ili ziwabebe kwenye muziki wa tofauti na ilivyokuwa kwa wasanii wa zamani.

“Wasanii wengi wa kuimba sasa wamekuwa wakitumia kiki wasanii wengi wamekuwa wakiwaiga wasanii wa Ulaya kutengeneza kiki kama hizo tofauti na wasanii wa zamani wengi walikuwa hawafanyi hivyo lakini muziki wao ulikuwa ukieleweka vizuri,” amekiambia kipindi cha Enews cha EATV.

Rapper huyo ameongeza kuwa kwa wale wasanii wanaotegemea kiki ipo siku watapotea vibaya na watabaki wasanii wanaofanya muziki mzuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni